Bibi Titi Mohammed (1926 - 5 Novemba 2000) alikuwa mmoja wa wanawake wa kwanza mzalendo kushika nafasi za ubunge na uwaziri nchini Tanzania. Pia alikuwa kati ya wanawake wa kwanza kujiunga na harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.[1]
Mwaka 1969 Bibi Titi Mohammed alikamatwa na mwaka uliofuata alifikishwa mahakamani kwa kosa la kula njama ya kutaka kupindua serikali. Katika kesi hiyo, Bibi Titi alikuwa ni mwanamke pekee katika washtakiwa 7. Baada ya kesi hiyo kusikilizwa alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha. Hata hivyo, mwaka 1972 alisamehewa na rais Julius Nyerere.
Nukuu
edit- Wanawake wanahitaji heshima, msaada na fursa sio huruma
- Haja ya kukusanyika pamoja na kutafuta sababu ya pamoja ya uhuru wetu ni sasa, lazima tuinuke kwa ajili ya Tanzania
- Bibi Titi Mohammed [1]