Wq/sw/Asha-Rose Migiro

< Wq | sw
Wq > sw > Asha-Rose Migiro

Asha-Rose Migiro (1956) aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Alipewa cheo hicho na Katibu Mkuu Ban Ki-moon tarehe 5 Januari 2007.

Asha-Rose Migiro

Hadi kuteuliwa kwa cheo cha UM alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania tangu Januari 2006. Wajibu huo alipewa na rais Jakaya Kikwete aliyemteua kumfuata katika Wizara ya mambo ya nje iliyoshikwa awali na Kikwete mwenyewe.

Chini ya rais Benjamin Mkapa Migiro alikuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto. Alikuwa mbunge kwa njia ya kiti maalumu cha wanawake.

Kabla ya kujiunga na siasa alifundisha kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Alisoma Shahada ya Awali na Shahada ya uzamili hukohuko Dar es Salaam

Nukuu

edit
  • Hakuna mahali popote duniani ambapo mwanamke yuko salama kutokana na ukatili. Kuimarika kwa dhamira ya kimataifa ya kukabiliana na janga hili ni vuguvugu ambalo wakati wake umefika
  • Nukuu za Asha-Rose Migiro

Viungo vya nje

edit