Wq/sw/Ali Hassan Mwinyi

< Wq | sw
Wq > sw > Ali Hassan Mwinyi

Ali Hassan Mwinyi (8 Mei 1925 - 29 Februari 2024) alikuwa Rais wa pili wa Tanzania kuanzia mwaka 1985 hadi 1995. Aliyemtangulia ni Mwalimu Julius Nyerere, na aliyemfuata ni Benjamin Mkapa. Pia alikuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia mwaka 1990 hadi 1996.

Ali Hassan Mwinyi

Nukuu

edit
  • Leo nina miaka karibu 94, sina siku nyingi za kuiacha dunia. Sitaki niende huko napoenda na aibu nyuma yangu.Maisha ya mwanadamu ni hadithi tu hapa ulimwenguni, basi ewe ndugu yangu kuwa hadithi nzuri kwa hao watakaosimuliwa…
  • Wakati wa uongozi wangu kulitokea vurugu zinazofanana na hizo baada ya watu kuvunja mabucha ya nguruwe, ambayo yalikuwa yanakwaza wale wanaofuata Dini ya Kiislamu. Niliwaambia wananchi ‘ruksa’ kula chochote watakacho, pia nilikuwa sitaki imani ya mtu mmoja kumuudhi mwingine, au ivunje sheria.
    • Haya ni maneno ya Rais mstaafu wa Awamu ya Pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi, aliyepata pia kuwa Rais wa Zanzibar. Vurugu hizo ndizo zilisababisha akapewa jina la utani la ‘Mzee Ruksa’ Soma zaidi hapa